Thursday, December 8, 2011

ROONEY APUNGUZIWA ADHABU.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza Wayne Rooney amepunguziwa adhabu yake ya kufungiwa michezo mitatu baada ya kukata rufani katika Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA nchini Switzerland. Adhabu hiyo ya Rooney ilipunguzwa kutoka michezo mitatu mpaka miwili ambapo adhabu ya mchezo wa tatu sasa atatakiwa kuitumikia ndani ya miaka minne hivyo kumwezesha kucheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi Ukraine katika michuano ya Kombe la Ulaya mwakani. Meneja wa Uingereza Fabio Capello aliungana na Rooney kusikiliza rufani hilo iliyokuwa ikisikilizwa na jopo la maofisa watatu wa UEFA leo asubuhi. Rooney ambaye ameichezea Uingereza mara 73 na kufunga mabao 28 alifungiwa na shirikisho hilo kufuatia kumchezea vibaya mchezaji timu ya Montenegro katika mchezo wa mwisho wa kutafuta tiketi ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment