Wednesday, December 7, 2011
NEYMAR MCHEZAJI BORA LIGI YA BRAZIL.
MSHAMBULIAJI wa Santos Neymar da Silva amepigiwa kura kuwa mchezaji bora wa mwaka katika Ligi Kuu ya Brazil. Neymar mwenye umri wa miaka 19 amefunga mabao 13 katika michezo 21 aliyochezwa hivyo kupelekea kushinda tuzo hiyo akiwazidi wachezaji wenzake ambao ni beki wa Vasco da Gama Dede na mshambualiaji wa Corinthians Liedson. Mshambuliaji huyo anayewaniwa na klabu mbalimbali za Ulaya hakuwepo kupokea tuzo yake hiyo kwasababu timu ilikuwa tayari imesafiri kuelekea Japan kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Klabu Bingwa la Dunia. Corinthians ndio wamenyakuwa ubingwa wa Brazil msimu huu ukiwa ni ubingwa wao wa tano wakifuatiwa na Vasco da Gama wakiwa na alama mbili nyuma yao wakati Santos na Palmeiras ambazo zimemaliza katika nafasi ya sita na saba zikiwa ndio klabu zenye mafanikio zaidi katika ligi hiyo baada ya kunyakua taji hilo mara nane kila mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment