Wednesday, September 7, 2011

BAADA YA MGOMO SASA SERIE A KUANZA KUTIMUA VUMBI IJUMAA.

MILAN, Italia
RAIS wa kamati ya usimamizi wa ligi ya nchini Italia Maurizio Beretta amewaambia waandishi wa habari kwamba ni furaha kubwa sana kwao kumaliza matatizo yaliyokua yanawakabili na sasa wanachosubiri ni kuona ligi inaanza kuchezwa katika viwanja mbali mbali.

Kiongozi huyo amedai kwamba mkataba walioingia na chama cha wachezaji upo wazi kwa kila mmoja wao, na hadhani kama kutakua na malalamiko tena mpaka mwezi June mwaka 2012 ambapo itakua mwisho wa mkataba huo.

Nae Rais wa chama cha wachezaji nchini Italia Damiano Tommasi amesema kama uongozi wa kamati ya kusimamia ligi umedhihirisha wazi makubaliano waliyofikia hakuna haja ya kuzungumza kwa kina zaidi ya kushukuru kwa kila jambo lilivyokua likipangwa katika mikutano yao.

Kumalizika kwa mgomo huo, kunaifanya ligi ya nchini Italia kuanza kuunguruma siku ya ijumaa ambapo mabingwa watetezi AC Milan watafungua kwa kucheza na SS Lazio katika uwanja wa San siro.

No comments:

Post a Comment