Wednesday, September 28, 2011

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL YASHINDA, CHELSEA YANG'ANG'ANIWA.

Mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain akishangilia pamoja na Arshavin mara baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza dhidi ya Olympiakos katika Uwanja wa Emirates ambapo Arsenal ilishinda 2-1.

Chamberlain akifunga bao la kwanza.

Adre Santos akiweka kimiani bao la pili la Arsenal katika mchezo huo.

Santos na Thomas Rosicky wakishangilia mara baada ya kufunga bao la pili.

Mshambuliaji wa olympiakos David Fuster akipiga kichwa kufunga bao la kufutia machozi la timu yake.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akizungumza na CEO wa  timu hiyo upande wa jukwaani ikiwa ni hatua ya kumalizia adhabu yake ya kufungiwa mechi mbili kutokukaa katika benchi la ufundi katika mchezo huo.

MATOKEO YA MICHEZO YA LEO.

Arsenal 2-1 Olympiakos
AC Milan 2-0 Plzen
BATE Borisov 0-5 Barcelona
Bayer Leverkusen 2-0 Genk
Marseille 3-0 Borussia Dortmund
Shakhtar Donetsk 1-1 Apoel Nicosia
Valencia 1-1 Chelsea

No comments:

Post a Comment