Monday, September 5, 2011

RONALDO AMVULIA KOFIA MESSI.

MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anafikiri kuwa mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi kuwa ndiye mchezaji bora duniani.

Ronaldo (26) aliulizwa kuhusu mawzo yake anamuonaje Muargentina huyo ndivyo akajibu hivyo, lakini aliendelea kusema kuwa mchezaji huyo ni wa aina ya peke yake.

"Ndiye mchezaji bora kwa sasa," alikaririwa Ronaldo kwa mujibu wa gazeti la Sport.

"Ana tabia zake nami nnazo zangu pia. Ana aina ya mchezo wake nami nnao wangu. Pia nacheza klabu kubwa kama yeye. Tuko tofauti kwa kila kitu." alimalizia Ronaldo.

Maelezo yake hayo yamekuja siku chache baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kudai kuwa klabu yake ya sasa ya Madrid ndiyo bora duniani kwa sasa.

No comments:

Post a Comment