Friday, February 17, 2012

BECKHAM AMKINGIA KIFUA CAPELLO.

NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza David Beckham yupo pamoja na Fabio Capello kufuatia uamuzi wake wa kujiuzulu wadhifa kama meneja wa timu hiyo. Beckham akihojiwa kwa mara ya kwanza toka kujiuzulu kwa kocha huyo amesema kuwa amesikitishwa na kitendo cha Capello kujiuzulu nafasi yake hiyo katika kipindi ambacho ni karibu na michuano ya Kombe la Ulaya lakini akasema kuwa anaheshimu uamuzi wake kwani anaamini kocha lazima apewe nafasi ya kuteua nahodha wake mwenyewe. Mchezaji huyo aliendelea kusema amefanya kazi na Capello kwa miaka michache hivyo inasikitisha kuona anaondoka katika kipindi hiki muhimu ambacho timu ya Uingereza inakabiliwa nacho. Capello aliachia wadhifa wake huo wiki iliyopita baada ya kufanya mkutano na Chama cha Soka cha Uingereza-FA ambapo walivua unahodha John Terry kufuatia kashfa ya kumtutolea maneno ya kibaguzi beki wa Queens Park Rangers Anton Ferdinand.

No comments:

Post a Comment