Friday, February 17, 2012

VILLAR ACHAGULIWA TENA KUONGOZA RFEF.

Angel Maria Villar amechaguliwa tena bila kupingwa kwa mara ya saba kuongoza kwa miaka mingine minne kama rais wa Shirikisho la Soka nchini Hispania-RFEF huku kukiwa na madai ya kukiuka taratibu za uchaguzi. Villar mwenye umri wa miaka 62 ambaye ndiye Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA alikuwa ndiye mgombea pekee katika uchaguzi huo uliofanyika makao makuu ya RFEF jijini Madrid akiwa amepata kura 161 kati ya 167 ambapo kura tano ziliharibika na moja pekee ndio iliyompinga. Mahakama moja nchini Hispania ilitupilia mbali katika dakika za ombi la kusogeza uchaguzi huo mbele lililotolewa na Ignacio del Rio ambaye ni diwani wa zamani wa jiji la Madrid ambaye alikuwa akimtuhumu Villar na RFEF kukiuka taratibu za uchaguzi. Mshindi wa uchaguzi huo Villar pamoja na Rais wa UEFA Michel Platini walikuwa wkaifuatilia uchaguzi wakiwa katika msari wa mbele ambapo alishukuru wapiga kura wote pamoja na Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque kwa ushirikiano walioonyesha na kusema kuwa uchaguzi huo unafaa kuigwa na vyama vya soka duniani kote.

No comments:

Post a Comment