Friday, February 17, 2012

MEZZARRI KUWAKOSA CHELSEA.

KOCHA wa klabu ya Napoli ya nchini Italia Walter Mezzarri atakosa michezo miwili ya timu yake katika michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Ulaya hatua ya timu 16 bora dhidi ya Chelsea baada ya kushindwa rufani yake ya kufungiwa michezo miwili Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA. Mezzarri alifungiwa Januari baada ya kumsukuma mshambuliaji wa Villarreal Nilmar wakati wa mchezo wa Kundi A Desemba 7 mwaka jana ambapo timu yake ilishinda mabao 2-0 na kufanikiwa kuingia hatua hiyo. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 hatakuwepo katika benchi la ufundi la timu yake itapopambana na Chelsea Februari 21 pamoja na mchezo wa marudiano utakaochezwa Machi 14 mwaka huu. Pia kocha huyo amezuiliwa kuongea na wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi kabla ya mchezo na wakati wa mchezo pamoja na kutumia simu kuwasiliana na benchi lake la ufundi.

No comments:

Post a Comment