Tuesday, February 28, 2012

VAN DER VAART AACHWA KIKOSI CHA UHOLANZI.

KIUNGO wa kimataifa wa Uholanzi Rafael van der Vaart ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitacheza na Uingereza katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki Jumatano. Chama cha Soka nchini humo-KNVB kimesema katika taarifa yake kuwa kuingo huyo anayekipiga katika klabu ya Tottenham Hotspurs aliumia kifundo cha mguu mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akishuhudia kikosi chake kikipokea kipigo kutoka kwa mahasimu wao Arsenal chwa mabao 5-2. Mchezo baina ya timu hizo unatarajiwa kuchezwa nchini Uingereza katika Uwanja Wembley jijini London. Van der Vaart anakuwa mchezaji wa pili wa Uholanzi kuondolea katika kikosi hicho baada ya mlinda mlango wa kikosi hicho Michel Vorm nae kuondolewa kutoka kuugua.

No comments:

Post a Comment