Tuesday, February 28, 2012

PETR CECH MCHEZAJI BORA WA MWAKA NCHINI KWAO.

MILINDA mlango mkongwe wa kimataifa wa kutoka Jamhuri ya Czech Petr Cech ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo na kufikia rekodi ya kushinda tuzo hiyo kwa mara ya tano. Cech ambaye ana umri wa miaka 29 ameichezea timu ya taifa ya nchi hiyo mara 88 akiwa kama mlinda mlango wa kutegemewa na amekuwa na mafanikio makubwa katika klabu yake ya Chelsea anayochezea. Mchezaji ambaye amewahi kushinda tuzo hiyo mwaka 2005, 2008, 2009, 2010 na sasa 2012 alifanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji wenzie ambao ni kiungo anayekipiga katika klabu ya VfL Wolfsburg ya Ujerumani Petr Jiracek na Tomas Rosicky anayecheza Arsenal. Tuzo hizo ambazo hutolewa kila mwaka nchini humo hupigiwa kura na wachezaji, makocha, viongozi wa soka na waandishi wa habari za michezo.

No comments:

Post a Comment