BARCA YALIPWA FIDIA.
KITUO kimoja cha radio nchini Hispania kimeondoa tangazo ambalo lilitumika mwaka jana likidai kuwa wachezaji wa Barcelona wanatumia madawa haramu yaliyopigwa marufuku michezoni na kukubali kulipa kiasi cha euro laki mbili kama fidia. Katika taarifa ya kituo hicho waliyoweka katika mtandao wake Jumanne imesema kuwa tuhuma hizo ambazo zilitoka Machi mwaka jana zimeonyesha kuwa hazina ukweli wowote kuhusu wachezaji hao kutumia madawa hayo. Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa kituo hicho kimegundua kuwa kitendo walichofanya ni kinyume na sheria na wamelichafua jina klabu hiyo kwa namna moja au nyingine na kwa hilo wanaomba radhi. Tuhuma hizo ambazo klabu ya Barcelona ilikanusha na kutaka ziondolewe zilileta mkanganyiko baada ya vyombo vya habari nchini humo kudai kuwa aliyetoa taarifa hizo ni mmoja wa maofisa wa mahasimu wakubwa wa klabu hiyo klabu ya Real Madrid ambaye hajajulikana
No comments:
Post a Comment