Wednesday, February 29, 2012

CORINTHIANS YAMNYAKUA NYOTA KUTOKA CHINA.

KLABU ya Corinthians ya Brazil imemsajili kiungo wa kimataifa kutoka China Chen Zhizhao wakiamini kuwa mchezaji huyo atawasaidia kuwatangaza katika nchi hiyo ya bara la Asia. Chen ameshawahikucheza katika klabu ya nchini kwao ya Nanchang Hengyuan na pia kabla ya kwenda Corinthians alikuwa nchini Ureno akikipiga katika klabu ya Trofense. Wazo la kumyakuwa mchezaji huyo lilitoka idara ya masoko ya klabu hiyo ambapo wanajaribu kuifanya klabu hiyo kujulikana zaidi nje ya nchi hiyo. Idara hiyo ya masoko ya klabu hiyo pia ndio iliyotoa wazo la kumsajili Ronaldo de Lima miaka michache iliyopita wakati nyota huyo wa zamani wa Brazil alipokuwa akiuguza majeraha ya mguu wakati akiicheza klabu ya Ac Milan ya Italia.

No comments:

Post a Comment