Tuesday, February 21, 2012

LANDI ATIMULIWA LIBERIA.

SHIRIKISHO la Soka nchini Liberia-LFA limemfukuza kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Roberto Landi ikiwa ni wiki moja tu kabla timu hiyo haijaanza kampeni yake ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka ujao. Katika taarifa iliyotolewa na rais wa LFA Musa Bility alithibitisha kuondolewa kwa kocha huyo ambaye amekuwa akikinoa kikosi hicho kwa miezi 11. Sababu haswa za kumtimua kocha huyo hazikuwekwa wazi lakini timu hiyo imeshinda michezo miwili kati ya nane iliyocheza chini ya Landi na kipigo walichopata kutoka kwa timu ya Nigeria ambayo ilikuwa haina nyota wake wanaocheza ndizo zinatajwa kuwa sababu kubwa ya kutimuliwa na kocha huyo. Thomas Kojo ndio amepewa nafasi ya kushika nafasi ya Landi katika mchezo wa kwanza dhidi ya Namibia Jumatano wakati wakitafuta kocha atakayeziba nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment