Tuesday, February 21, 2012

FORLAN ATAMANI CHAMPIOS LEAGUE.

MSHAMBULIAJI wa Inter Milan Diego Forlan amedai kuwa ana hamu kubwa ya kucheza kwa mara ya kwanza michuano ya Klabu Bingwa ya Ulaya akiwa na kikosi hicho katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Olympique de Marseille utakaofanyika katika Uwanja wa Velodrome nchini Ufaransa Jumatano. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid alishindwa kucheza michuano hiyo katika hatua za makundi kutokana na sheria za Shrikisho la Soka Barani Ulaya lakini sasa anaweza kurejea tena kwenye mashindano hayo. Akihojiwa na mtandao wa Shrikisho la Soka barani Ulaya-UEFA Forlan amesema kuwa alikuwa na hamu kubwa ya kucheza michuano hiyo ambayo ni muhimu duniani na sasa anaeza kucheza huku timu yake ikiwa imeingia katika hatua timu 16 bora. Forlan aliendelea kusema kuwa katika michuano hiyo kuna timu nyingi ngumu hivyo inatakiwa kuchukulia kila mchezo na umuhimu wake na kupunguza kuweka matumaini ya kushinda juu.

No comments:

Post a Comment