Monday, February 20, 2012

GATTUSO ADAI YUKO TAYARI KUCHEZA BURE MILAN.

KIUNGO wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa yuko tayari kucheza bila kulipwa chochote pindi ataporejea uwanjani baada ya kuuguza jeraha la jicho linalomsumbua. Gattuso hajaichezea timu hiyo toka agongane na mchezaji mwenzie Alessandro Nesta katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A Septemba 9 mwaka jana. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 unaisha mwishoni mwa msimu huu lakini mchezaji huyo alimwambia rais wa klabu hiyo Adriano Galliani kuwa yuko tayari kucheza bila malipo yoyote kwani anachikitaka yeye akirudi ni kufanya kile anachokipenda. Gattuso amekuwa na klabu hiyo toka mwaka 1999 na ameshinda kila kitu akiwa na klabu hiyo pamoja na Kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa na timu ya taifa ya Italia. Mchezaji huyo amesema akiwa na umri wa miaka 34 hajafikiria chochote kuhusu kutundika daruga kwani anaishi kwa ajili ya soka.

No comments:

Post a Comment