Monday, February 20, 2012

QATAR YAPATA KOCHA MPYA.

Shirikisho la Soka nchini Qatar limeteua Paulo Autuori raia wa Brazil kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya mbio za kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Autuori ambaye alikuwa kocha wa timu ya Olimpiki ya nchi hiyo anakuwa kocha wa nne ndani ya mwaka mmoja kuinoa klabu hiyo ambayo imepania kupanda katika orodha za timu bora duniani ambapo kwasasa wanashika nafasi ya 96 kwasababu ndio watakaokuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Kocha huyo amewahi kuifundisha timu ya taifa ya Peru na klabu mbalimbali nchini Brazil ikiwemo klabu ya Sao Paulo ambayo aliiwezesha kunyakuwa Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia mwaka 2005 pia amefundisha baadhi ya vilabu nchini Qatar. Kazi ya kwanza ambayo itamkabili Autuori ni kukiongoza kikosi hicho katika mchezo wa mzunguko wa mwisho wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia ambapo katika kundi lao timu hiyo inashika nafasi ya pili huku ikikabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Iran Februari 29 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment