Tuesday, February 21, 2012

KESI YA BIN HAMMAM KUSIKILIZWA APRIL.

Rufani ya aliyekuwa mgombea urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Mohamed bin Hammam imetajwa kusikilizwa April 18 na 19 mwaka huu na Mahakama ya Michezo ya Usuluhishi-CAS akipinga kufungiwa maisha na shirikisho hilo kufuatia kashfa ya rushwa. Bin Hammam ambaye amekana makosa hayo hii inakuwa ni rufani yake ya pili ya kwanza ikiwa ni kusimamisha Shirikisho la Sola barani Asia-AFF kupinga kuondolewa nafasi yake kama rais wa Shirikisho hilo. FIFA ilimfungia Bin Hammam Julai mwaka jana baada ya Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo kumkuta na makosa ya kujaribu kununua wapiga kura wa Caribbean wakati wa uchaguzi wa ambapo alikuwa akipambana na Sepp Blatter. Bin Hammam ambaye ni raia wa Qatar alijitoa katika kinyang’anyiro hicho kufuatia kashfa hiyo Mei mwaka jana na sasa amekuwa akipambana na rufani yake aliyokata CAS ili kuzuia uchaguzi wa AFF unaotarajiwa kufanyika Mei mwaka huu.

No comments:

Post a Comment