Tuesday, February 21, 2012

BERETTA APEWA MIKOBA YA KUINOA CESENA

MARIO Beretta ameteuliwa kuinoa klabu ya Cesena ya nchini Italia baada ya kuchuklua nafasi ya kocha aliyetimuliwa Daniele Arrigoni ambapo anakuwa kocha wa tatu kuinoa klabu hiyo toka msimu huu ulipoanza. Arrigoni alitimuliwa kuinoa klabu hiyo jana ikiwa ni siku moja baada ya timu hiyo kupokea kipigo cha mabao 3-1 wakiwa uwanja wao wa nyumbani dhidi ya AC Milan ambapo nae alichukua nafasi ya Marco Giampaolo aliyetimuliwa mapema Novemba mwaka jana. Hatahivyo klabu hiyo imeshinda mchezo wake mmoja tu kati ya michezo 10 iliyocheza hivi karibuni na kuifanya kushika mkia katika Ligi Kuu nchini Italia wakihitaji alama saba ili kujinasua katika hatari ya kushuka daraja. Kabla ya kutua Cesena Beretta aliwahi kuinoa klabu ya Brescia msimu uliopita lakini alitimuliwa ndani ya miezi miwili na klabu hiyo ambayo hatahivyo ilishuka daraja.

No comments:

Post a Comment