Tuesday, February 21, 2012

IVORY COAST YAIPONGEZA ZAMBIA.

SHIRIKISHO la Soka la Ivory Coast-FIF limetuma barua ya pongezi kwa maningwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika Zambia baada ya timu hizo kucheza hatua ya fainali ya michuano hiyo iliyofanyika Februari 12 mwaka huu. FIF walitoa pongezi zao kwa kiwango bora kilichoonyeshwa na timu hiyo maarufu kama Chipolopolo na kusifu kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu na mzuri ambao Afrika na dunia nzima walifurahia. Katika barua hiyo ambayo rais wa FIF Augustine Sidy Diallo alimtumia rais wa Shirikisho la Soka la Zambia-ZFF Kalusha Bwalya aliwasifu Chipolopolo kwa kunyakuwa ubingwa huo kwa kudai kuwa walionyesha kiwango bora na walistahili ushindi katika mchezo huo. Diallo aliendelea kusema kuwa ushindi huo wa Zambia ulichochewa na umoja na ushirikiano waliokuwa nao wachezaji pamoja na uongozi mzima wa shirikisho la nchi hiyo pamoja na mashabiki kwa ujumla. Zambia walifanikiwa kuwafunga Ivory Coast kwa changamoto ya mikwaju ya penati 8-7 baada ya kushindwa kufungana katika muda wa kawaida na kutawadhwa kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment