Monday, February 13, 2012

RANGERS MBIONI KUFILISIKA.

Klabu ya soka ya Rangers imethibitisha kwamba imewasilisha ombi lake kisheria mahakamani ikiwa na nia ya kupata watu watakaosimamia shughuli za klabu huku ikijitayarisha kutangaza kufilisika. Klabu hiyo imetangaza kwamba itaendelea na shughuli zake kama kawaida, hadi itakapotangaza uamuzi wa mwisho kama itaendelea na hatua hiyo. Rangers sasa ina siku 10 kufanya uamuzi na wakati hayo yakiendelea klabu imetangaza kwamba mashabiki wenye tiketi za msimu mzima, na vile vile wenye hisa, wasiwe na wasiwasi wowote. Hatua hiyo imechukuliwa huku Rangers ikisubiri uamuzi kuhusiana na utata juu ya ushuru, pamoja na faini mbalimbali ambazo klabu hiyo inadaiwa na jumla ya deni likiwa ni pauni milioni 49. Katika taarifa iliyotilewa na klabu hiyo imeelezea kwamba ikiwa uamuzi huo utaamuliwa kwa idara ya forodha kushinda kesi basi itamaanisha malimbikizo ya deni hilo na faini huenda yakazidi hata pauni milioni 50 na klabu hakitakuwa na uwezo wa kulilipa deni hilo. Tajiri anayemiliki klabu hiyo Craig Whyte alinukuliwa baadaye akisema deni hili huenda likazidi na kufikia pauni milioni 75. Whyte, ambaye alinunua klabu kutoka kwa Sir David Murray mwaka jana, alisema suala la klabu kupata usimamizi mpya ni jambo la kufikiriwa iwapo klabu itashindwa katika kesi hiyo kuhusiana na ushuru.

No comments:

Post a Comment