Monday, February 13, 2012

ZAMBIA YAPOKEWA KISHUJAA.

TIMU ya Taifa ya Zambia imewasili nchini mwao Jumatatu na kupata mapokezi ya hali ya juu kutoka kwa zaidi ya maelfu ya mashabiki waliojitokeza kuwalaki mashujaa wao baada ya kunyakuwa taji la kwanza la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Wakiwa na kombe hilo walilopata baada ya kuifunga Ivory Coast kwa changamoto ya mikwaju ya penati Jumapili iliyopita mabingwa hao wapya wa Afrika waliwapungia mkono mashabiki walijitokeza kuwalaki katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka. Baadae kikosi hicho kilipanda basi kuelekea katika uwanja wa maonyesho wa Lusaka ambapo mashabiki wanaokadiriwa kufikia 200,000 wakiwa wamevaa jezi za timu ya taifa ya nchini hiyo walikuwa wamekusanyika kwa ajili sherehe maalumu iliyoandaliwa. Mashabiki hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali wakati wengine wakipuliza mavuvuzela na mara kikosi hicho kiliowasili polisi walipata wakati mgumu kuwatuliza mashabiki hao ambao kila mmoja alikuwa nataka kuwaona mashujaa wao hao.

No comments:

Post a Comment