Saturday, February 18, 2012

WENGER AOMBA RADHI MASHABIKI WA KLABU HIYO.

MENEJA wa Klabu ya Arsenal Arsene Wenger amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kufuatia kipigi cha mabao 4-0 walichopata toka kwa AC Milan katikati ya wiki katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya. Akihojiwa kabla ya mchezo wa Kombe la Chama cha Soka cha Uingereza-FA dhidi ya Sunderland utakaopigwa leo Wenger amesema kuwa mashabiki walikuwa upande wao katika muda wote walipokuwa wanacheza na Milan ndio maana anaomba samahani kwa mashabiki hao kwa matokeo ambayo hayakuridhisha. Akizungumzia mchezo wa leo dhidi ya Sunderland Wenger amesema mchezo huo utakuwa ni vita nyingine ambayo wanahitajika kupambana hivyo aliwaomba mashabiki kushangilia timu yao hiyo ili waweze kufanya vizuri. Arsenal imeshindwa kushinda kikombe chochote kwa miaka saba huku wakiwa hawana matumaini ya kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kipigo walichopata kutoka Milan hivyo mchezo wa leo utakuwa muhimu ili kuweka matumaini ya kunyakuwa kombe la FA.

No comments:

Post a Comment