Saturday, February 18, 2012

GHANA KUCHEZA NA CHILE.

TIMU ya taifa ya Ghana maarufu kama Black Stars wanatarajia kucheza mchezo wa kimataifa wa maonyesho wa kirafiki dhidi ya timu ya Chile Februari 29 mwaka huu jijini Philadelphia, Marekani. Mchezo baina ya timu hizo ulitangazwa jana na upo katika kalenda ya kimataifa ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA hivyo kuna uwezekano mkubwa vikosi vya timu zaote mbili vikaita nyota wao wanaocheza klabu mbalimbali Ulaya. Moja ya majina ya nyota wanaotarajiwa kuwepo katika timu ya Chile ni pamoja na mshambuliaji wa Barcelona Alexis Sanchez na Humberto Suazo anayekipiga Monterrey wakati Ghana wanatarajia kuwa na nyota wao kama Michael Essien anayekipiga Chelsea na Andre Ayew anayecheza Marseille ya Ufaransa. Ghana ambao walifika hatua ya nusu fainali katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyoandaliwa kwa pamoja na Guinea ya Ikweta na Gabon waliifunga timu ya taifa ya Marekani kwa mabao 2-1 kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 na kufanikiwa kuingia mzunguko wa pili wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment