Saturday, February 18, 2012

DUARTE ATIMULIWA BURKINA FASO.

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Burkina Faso Paulo Duarte ametimuliwa kibarua chake hicho kufuatia uamuzi ulifikiwa na Shirikisho la Soka la nchini hiyo-FBF. Uamuzi wa kumtimua kocha huyo raia wa Ureno ulifikiwa baada ya matokeo mabaya iliyopata timu hiyo katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kupoteza michezo yote mitatu katika kundi B walilopangwa hivyo kuwafanya kutolewa katika hatua za mwanzoni za michuano hiyo. Mwenyekiti wa FBF Zambede Theodore Sawadogo alithibisha suala la kusitisha mkataba na kocha kocha ambapo amesema kuwa aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi hicho ndiye atakayekinoa kikosi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Morocco Februari 29 mwaka huu wakati wanafanya mchakato wa kutafuta mbadala wa Duarte. Duarte mwenye umri wa miaka 42 ambaye alikuwa akifananishwa na kocha wa timu ya Real Madrid Jose Mourinho alikuwa akiinoa klabu hiyo toka mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment