Saturday, February 18, 2012

WARNER KUSHITAKIWA TRINIDAD & TOBAGO.

SHIRIKISHO la Soka la Trinidad na Tobago limesema liko katika mpango wa kumfungilia mashtaka aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Jack Warner kwa ajili ya kurudisha fedha za msaada zikiwemo zile za janga la tetemeko la ardhi nchini Haiti. Wakili wa Shirikisho hilo Derek Ali alimwambia Jaji kuwa wanampango wa kumfungulia mashtaka Warner kwa kushindwa kuachia fedha hizo zilizotolewa wakati ambao alikuwa kama mshauri maalumu wa shirikisho hilo kabla ya kujiuzulu mwaka uliopita kufuatia kashfa ya rushwa. Jaji wa mahakama kuu nchini humo Devindra Rampersad alimpa maagizo Ali kumpelekea barua Warner juu ya uamuzi wa shirikisho hilo. Akihojiwa juu ya suala hilo na waandishi wa habari Warner alijibu kwa kifupi kuwa hiyo ni haki yao ya msingi kufanya hivyo akawaomba waandishi kuwa na uvumilivu katika hili kuangalia nini kitatokea baadae.

No comments:

Post a Comment