Thursday, February 23, 2012

ROONEY KUIKOSA AJAX.

KLABU ya Manchester United imesema kuwa mshambuliaji wake Wayne Rooney atakosa mchezo wa Ligi ya Vilabu barani Ulaya dhidi ya Ajax Amsterdan ya Uholanzi leo kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya koo. Rooney alianza kuumwa baada ya timu yake hiyo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ajax nchini Uholanzi katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo. Meneja wa United Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa mchezaji huyo anaumwa koo na kuongeza kuwa dalili za ugonjwa huo zilianza kuonekana toka katika mchezo waliocheza Amsterdam akapatiwa matibabu lakini hayakusaidia kwani hali iliendelea kuwa mbaya. Mbali na mchezo huo dhidi ya Ajax United pia inakabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Norwich na Ferguson amesema kuwa wanafanya kila wawezalo kuhakikisha anakuwa fiti kabla ya Jumapili.

No comments:

Post a Comment