Monday, February 27, 2012

MTUKUTU BALOTELLI AACHWA ITALIA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Italia Mario Balotelli ameachwa na kocha wa timu taifa ya nchi hiyo Cesar Prandelli kutokana na tabia za utovu wa nidhamu awapo uwanjani. Mshambuliaji huyo anayekipiga katika klabu Manchester City ya nchini Uingereza nafasi yake imechukuliwa na mshambuliaji anayecheza katika klabu ya AS Roma mwenye miaka 20 kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Marekani jijini Genoa. Balotelli amefungiwa kucheza michezo minne baada ya kumpga kofi kwa makusudi beki wa timu ya Tottenham Hotspurs Scott Parker Januari mwaka huu. Akihojiwa kuhusu uamuzi wa kumuacha mchezaji huyo Prandelli amesema kuwa katika kikosi chake hahitaji mchezaji ambaye anafanya makosa ambayo yanamsababisha atolewe nje hivyo kwake yeye haoni kama atakuwa na mchango katika kikosi chake. Mchezaji huyo ameshatolewa mara tatu toka ajiunge na City kwa ada ya paundi milioni 24 akitokea katika klabu Inter Milan Agosti mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment