Monday, February 27, 2012

MARADONA KUTEMBELEA KAMBI YA AL AHLY.

NGULI wa soka wa zamani Diego Armando Maradona anatarajiwa kutemebelea kambi ya timu ya Al Ahly ambayo wameweka huko Falme za Kiarabu-UAE ambapo vyombo vya habari nchini humo vimesema ziara hiyo itakuwa ni kuwapa moyo wachezaji wa timu kutokana na tukio liliwakuta hivi karibuni. Mjumbe mmoja wa bodi ya Al Ahly ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema hawana uhakika sana kama Maradona atawatembelea lakini wanaamini kama atawatembelea na kuongea na wachezaji itasaidia kuwatia moyo wachezaji kutokana na tukio lilitokea nchini Misri. Maradona kwasasa ni kocha wa Al Wasel ya Dubai baada ya kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo msimu uliopita. Wakiwa huko kambini Al Ahly wanatajiwa kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na vilabu vya huko ikiwemo timu Al Ahly ya Dubai, Al Kuwait na nyingine ambazo zitatajwa hapo baadae.

No comments:

Post a Comment