Thursday, February 23, 2012

NIGER NAYO YATIMUA KOCHA WAKE.

SHIRIKISHO la Soka nchini Niger-Fenifoot limemtimua kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Hamidou Doula na kumpitisha msaidizi wake Rolland Courbis ambaye ni raia wa Ufaransa kuchukua nafasi hiyo. Courbis alikuwa ameajiriwa kumsaidia Doula ambaye aliisaidia timu hiyo kukata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika lakini makocha hao walipishana kauli wakati wa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Gabon ambapo Courtis alimtuhumu Doula kwa kupanga kikosi kisicho sahihi. Fenifoot walikubaliana na Courtis ambaye pia aliwahi kuinoa klabu ya Marseille ya Ufaransa na kumpa kibarua hicho cha kukiongoza kikosi hicho katika michezo inayowakabili huko mbeleni. Niger ilishindwa kushinda hata mchezo mmoja kati ya mitatu waliyocheza katika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Matifa ya Afrika na kuwa timu ya kwanza kung’olewa katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment