Thursday, February 23, 2012

MANCINI AMALIZA MGOGORO NA TEVEZ.

MENEJA wa Manchester City Roberto Mancini amemaliza mgogoro aliokuwa nao mwa muda mrefu na mshambuliaji wa klabu hiyo Carlos Tevez na kusisitiza kuwa sasa anaweza kumchagua mchezaji huyo katika kikosi chake. Lakini Mancini amesema baada ya timu hiyo kufika katika hatua ya timu 16 bora katika Kombe la Ligi la Vilabu vya Ulaya baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Porto mabao 4-0 kuwa Tevez inabidi afanye mazoezi kwa bidii kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza kama zamani. Mapema wiki hii Tevez aliomba msamaha kufuatia hatua yake ya kuondoka kikosini hapo bila kuaga na kuelekea kwao Argentina baada ya Mancini kumuondoa katika mipango yake baada ya kukataa kupasha misuli moto katika mchezo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich Septemba mwaka jana. Mancini ambaye ni raia wa Italia amesema kuwa hana tatizo na mchezaji huyo kwakuwa ameshaomba msamaha na anatarajia anatarajia kukutana nae kabla ya mazoezi kesho na baada ya hapo anaweza kuendelea na mazoezi na wenzake.

No comments:

Post a Comment