Wednesday, February 22, 2012

TEVEZ AOMBA RADHI.

Mshambuliaji wa Manchester United Carlos Tevez amewasilisha msamaha wake kwa Klabu hiyo na mashabiki wake kutokana na tabia alizozionyesha katika msimu huu. Tevez alitengeneza vichwa vya habari Octoba mwaka jana baada ya kukataa kupasha moto misuli alipotakiwa kufanya hivyo na Meneja Roberto Mancini wakati wa mchezo wa Klabu bingwa ulaya dhidi ya Bayern Munich uliofanyika katika Uwanja wa Allianz Arena. Muajentina huyo hajakichezea kikosi hicho cha Mancini tangu alipoamua kurejea kwao bila ruhusa kwa miezi mitatu huku akiwa katika jitihada za kuhamia AC Milan katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo mwezi Januari. Hata hivyo ameomba radhi kutokana na vitendo vyake na huenda akarejea katika kikosi cha kwanza cha City. Mshambuliaji huyo ametuma taarifa kupitia tovuti ya Klabu hiyo akiomba msamaha kwa wote aliowaangusha na kuathirika kutokana na vitendo alivyovifanya miezi iliyopita. Amesema kwasasa anataka kuelekeza mawazo yake kwa kucheza mpira katika Klabu ya Manchester City.

No comments:

Post a Comment