Wednesday, February 22, 2012

EUSEBIO AREJESHWA TENA HOSPITALI.

Mchezaji wa zamani wa Ureno Eusebio amerejea tena Hospitali kwa mara ya tatu ndani ya miezi miwili. Kwa mujibu wa Hospitali ya da Luz iliyopo Lisbon nyota huyo wa zamani wa Benfica alipelekwa Hospitalini hapo kutokana na kukabiliwa na shinikizo la damu. Madaktari wa Hospitali hiyo wamesema waliamua kubaki na Eusebio usiku baada ya kumfanyia vipimo vya mkojo siku ya Jumatatu na anatarajiwa kuruhusiwa ndani ya saa 48. Eusebio alishehereke sikukuu ya Christmas akiwa Hospitali kutokana na kukabiliwa na matatizo ya nimonia alirejeshwa tena Hospitali siku chache baadae kutokana na mamumivu ya shingo. Eusebio da Silva Ferreira ambaye amefikisha miaka 70 mwezi uliopita amekuwa nyota wa Ureno baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia katika miaka ya 1960 na alikuwa ni miongoni mwa wachezaji bora kumi wa muda wote mwaka 1998.

No comments:

Post a Comment