SHIRIKISHO la Soka barani Asia-AFC bado linaendelea na uchunguzi dhidi ya rais wa shirikisho hilo aliyesimamishwa Mohamed Bin Hammam pamoja na muda wa kusimamishwa kumalizika Jana. AFC inafanya uchunguzi kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya fedha aliyofanya Bin Hammam kipindi akiwa kiongozi wa shirikisho hilo. Katika taarifa iliyotolewa na AFC imesema kuwa pamoja na siku za kusimamishwa kuisha jana, Bin Hammam mwenye miaka 63 ambaye ni raia wa Qatar atandelea kutumikia adhabu yake ya siku 90 kutojishughulisha na soka aliyopewa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA . FIFA ilimfungia maisha Bin Hammam kujishughulisha na soka kutokana na makosa ya kutoa rushwa wakati alipokuwa akigombani nafasi ya urais wa shirikisho hilo mwaka uliopita lakini adhabu hiyo ilitenguliwa na Mahakama ya Kimataifa ua Usuluhishi wa Michezo Julai 19 mwaka huu. Baadae FIFA ilimfungia kwa siku 90 ili kuandaa ushahidi mpya juu ya tuhuma zinazomkabili Bin Hammam baada ya CAS kusema kuwa hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja kwamba mtuhumiwa alitoa rushwa. Bin Hammam alikana makosa yote hayo anayotuhumiwa na AFC na FIFA na kudai kuwa anajipanga na baadae atangaze hatua atakazozichukua kuhusiana na changamoto hizo zinazomkabili.
Wednesday, September 5, 2012
TANZANIA YAPOROMOKA TENA VIWANGO FIFA.
TANZANIA imeporomoka tena kwa nafasi nne katika viwango vya soka duniani vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutoka nafasi ya 128 waliyokuwepo mwezi uliopita mpaka nafasi ya 132. Mabingwa mara tano wa Kombe Dunia bado wamendelea kusota nje ya kumi bora baada ya kupanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 13 mwezi uliopita mpaka nafasi ya 12 baada ya kushinda mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Sweden. Katika orodha hizo mabingwa wa Ulaya na Dunia, Hispani bado wameendelea kuwa vinara katika orodha hiyo wakifuatiwa na Ujerumani waliopo katika nafasi ya pili huku Uingereza nao wakibakia katika nafasi yao ya tatu waliokuwepo msimu uliopita. Ureno imekwea nafasi moja kutoka nafasi ya tano waliyokuwepo mwwezi uliopita mpaka nafasi ya nne wakiwateremsha Uruguay mpaka nafasi ya tano wakati nchi za Italia inayoshika nafasi ya sita, Argentina saba, Uholanzi nane, Croatia tisa na Denmark 10 zikikamilisha kumi bora ya orodha hiyo kwa kubakia katika nafasi zao ambazo walikuwepo msimu uliopita. Kwa upande wa tano bora za Afrika Ivory Coast bado inaendelea kuongoza kwa kuwepo katika nafasi ya 16 wakifuatiwa na Algeria ambao wamepanda kwa nafasi sita mpaka nafasi ya 28 huku Ghana wakishika nafasi ya tatu kwa kupanda nafasi moja mpaka nafasi ya 32. Tano bora kwa Afrika inakamilishwa na nchi za mali ambao wamekwea kwa nafasi saba mpaka nafasi ya 32 na Libya ni watano wakiwa wamepanda nafasi mbili mpaka nafasi ya 36 waliyofikia mwezi huu.
FERGUSON KUMJARIBU BOLT KATIKA MCHEZO WA HISANI.
![]() |
| Ferguson akipiga stori na Bolt. |
![]() |
| Bolt akisakata kabumbu. |
Akihojiwa na gazeti la timu hiyo Ferguson amesema kuwa alizungumza na Bolt na kumuuliza kama anaweza kucheza mechi ya hisani na akamjibu kwamba anaweza, hivyo itakuwa ni jambo zuri kumtumia katika mchezo wa hisani dhidi ya Madrid ambao utapigwa Januari mwakani na kumuangalia kama ataweza.
MAN UNITED YAMTENGEA NEYMAR PAUNDI MILIONI 38.
KLABU ya Manchester United imetenga kitita cha paundi milioni 38 kwa ajili ya kumnyakuwa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar. Dau hilo ambalo linavunja rekodi ya klabu hiyo, ilishindwa wakati timu hiyo ilipomtaka mara ya kwanza baada ya nyota huyo mwenye miaka 20 anayecheza katika klabu ya Santos kusema kuwa anataka kubakia katika klabu yake hiyo mpaka baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 ambapo nchi yake itakuwa wenyeji. Nia ya meneja wa United Sir Alex Ferguson kutaka kumsajili Neymar kunazua maswali mengi juu ya mustakabali wa mshambuliaji wa klabu hiyo Wayne Rooney kwani kocha huyo ameonekana hawezi kushindwa kujaribu kumsajili Neymar tena katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. United imeamua kuhamishia nguvu zake kwa Neymar baada ya kuzidiwa kete na klabu ya Paris St Germain ya Ufaransa katika mbio za kumsajili Mbrazil mwingine Lucas Moura ambaye ana umri wa miaka 19. Ila bado inaonekana kutakuwa na vita kubwa ya kumgombani mchezaji huyo ambaye amefunga mabao 113 katika michezo 190 aliyochezea klabu ya Santos, kwani klabu za Real Madrid na Barcelona nazo zimeonyesha nia ya kumsajili.
SIJAOMBA FEDHA ZAIDI - RONALDO.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo amesema kuwa kukosa kwake furaha katika klabu hiyo hakuhusiani na mambo ya fedha kama baadhi ya vyombo vya habari vinavyosema kwani kikubwa anachotaka yeye ni mkataba wenye faida zaidi. Mshambuliaji huyo ghali zaidi duniani alitawala vyombo vya habari baada ya ushindi wa timu yake wa mabao 3-0 dhidi ya Granada Jumapili iliyopita wakati alipokataa kushangilia mabao mawili aliyofunga katika mchezo huo na baadae kusema kuwa alikuwa na huzuni. Ronaldo aliandika ujumbe katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa twitter kuwa kuonyesha uzuni aliyokuwa nayo kumezua mjadala mkubwa huku watu wakimtuhumu kuwa anahitaji pesa zaidi lakini siku moja watu hao watakuja kuona kwamba huzuni yake haihusiana na suala la kuongezwa fedha. Kuna taarifa pia zilizochapishwa na vyombo vya habari nchini humo kuwa mchezaji huyo alifanya mkutano na rais wa klabu hiyo Florentino Perez Jumamosi na kumwambia kuwa hadhani kama anapewa ushirikiano katika vyumba vya kubadilishia nguo, hana furaha na anataka kuondoka klabuni hapo. Ronaldo ambaye ni mojawapo ya wachezaji wanaolipwa zaidi duniani akikinga kiasi cha dola milioni 13 kwa mwaka, alikana tetesi zote hizo na kuwahakikishia mashabiki wa Madrid kwamba bado ana nia ya kubakia hapo na kushinda mataji zaidi.
Tuesday, September 4, 2012
RONALDO AZITAMANISHA MAN UNITED NA CITY.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameziweka klabu za Manchester United na City kujiweka tayari kumsajili baada ya kukiri kuwa anataka kuondoka Madrid. Chanzo kimoja cha habari nchini Hispania kilihabarisha kuwa nyota huyo alimwambia rais wa Madrid kuwa anataka kuondoka kwa kile kilichodaiwa kushindwa kuelewana na baadhi ya wachezaji wenzake. Hali hiyo ya kutokuwa na furaha kwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 27 ilionekana wazi wakati wa mchezo wa Jumapili baina ya Madrid na Granada ambapo alishinda mabao mawili lakini hakushangilia. Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo nyota huyo amesema kuwa alikuwa katika majonzi na viongozi wa klabu hiyo wanajua sababu hivyo hawezi kusema zaidi kuhusiana na hilo. Kauli hiyo inazitamanisha klabu za United, City pamoja na Chlesea kumsajili mchezaji huyo ambapo hivi sasa watakuwa wakifuatilia mstakabali wa mchezaji huyo katika klabu hiyo.
US OPEN: SERENA ATINGA ROBO FAINALI KWA KISHINDO.
MCHEZAJI nyota wa tenisi kutoka Marekani, Serena Williams amefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya wazi ya Marekani baada ya kumsambaratisha Andrea Hlavackova kwa 6-0 6-0. Serena ambaye ni bingwa mara tatu wa michuano hiyo atapambana na Ana Ivanovic aliyemfunga Tsvetana Pironkova kwa 6-0 6-4 katika mzunguko wa nne. Katika mchezo wa wawili wawili Serena na dada yake Venus Williams walishindwa kutamba mbele ya Maria Kirilenko na Nadia Petrova kutoka Urusi baada ya kufungwa kwa seti 2-0 za 6-1 6-4. Kwa upande wa wanaume Andy Murray wa Uingereza alifanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kumfunga Milos Raonic kwa 6-4 6-4 6-2.
Subscribe to:
Posts (Atom)







