Friday, January 4, 2013
YANGA KIBARUANI KESHO UTURUKI.
Timu ya Yanga kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na tim ua Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo utakaofanyika mjini Antalya majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati. Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo katika mji wa Antalya imekuwa ikifanya mazoezi tangu siku ya jumatatu na wachezaji wote wameonekana kufurahia mazingira ya kambi na huduma zote kwa ujumla. Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku tano (5) mfiululizo itatumia mchezo wa kesho dhidi ya timu ya Arminia Bielefed kama kipimo tosha cha maendeleo ya mafunzo yanayoendelea nchini Uuturuki. Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie Brandts amesema anashukuruika wachezaji wake wapo fit kwa ajili ya mchezo kesho, na kwa kuwa hakuna mchezaji majeruhi atakuwa na fursa ya kumtumi amchezaji yoyote katika mechi hiyo. Aidha Brandst amesema kuwa anajua mchezo wa kesho utakua mgumu kwani timu ya Arminia Bielefeld ni timu nzuri na imekua ikishiriki ligi kuu ya ujerumani mara kadhaa, hivyo ni timu ambayo itatoa ushindani mkubwa sana
TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.
STARS KUJIPIMA KWA ETHIOPIA JANUARI 11
Timu ya Taifa (Taifa Stars) itacheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Januari 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Addis Ababa, Ethiopia. Stars chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen inatarajia kuingia kambini jijini Dar es Salaam keshokutwa (Januari 6 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo. Mechi hiyo itakuwa kipimo cha mwisho kwa Ethiopia kabla ya kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazoanza Januari 19 mwaka huu. Ethiopia iko kundi C pamoja na mabingwa watetezi Zambia, Nigeria na Burkina Faso. Ethiopia itacheza mechi yake ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya Zambia. Katika mechi yake ya mwisho, Taifa Stars iliifunga Zambia bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Desemba 22 mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Ethiopia ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014. Mechi hiyo itachezwa Machi mwaka huu. Wachezaji wanaotakiwa kambini ni Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba). Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar). Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). Wakati benchi la Ufundi lina Kim, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
UCHAGUZI KWA WANACHAMA WA TFF
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inatarajia kukutana leo mchana (Januari 4 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itapitia maendeleo ya uchaguzi kwa wanachama wa TFF ikiwemo Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board). Wanachama wa TFF (vyama vya mikoa) wote wameshafanya uchaguzi ukiondoa mikoa ya Rukwa na Katavi inayotarajiwa kufanya uchaguzi baadaye mwezi huu. Kwa upande wa vyama shiriki ambavyo bado havijafanya uchaguzi ni Makocha (TAFCA), Wachezaji (SPUTANZA), Waamuzi (FRAT) na Tiba ya Michezo (TASMA). Vilevile Kamati ya Uchaguzi ya TFF baada ya kikao hicho huenda ikatangaza rasmi mchakato wa uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.

AYEW HATIHATI KUSHIRIKI AFCON.
KLABU ya Olympique Marseille ya Ufaransa imesema kuwa mshambuliaji wake nyota Andre Ayew ameumia goti wakati wa mazoezi Januari 2 ambapo waliliandikia Shirikisho la Soka la Ghana-GFA juu ya taarifa hizo. Habari za kuumia kwa Ayew zitakuwa ni pigo lingine kwa kocha wa timu ya taifa ya Ghana baada ya mshambuliaji wake mwingine kati ya wanne aliowateua kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon Yahaya Mohammed naye kuwa majeruhi. GFA nayo imewaagiza Marseille kumuachia Ayew kwenda jijini Abu Dhabi ili waweze kumfanyia uchunguzi wenyewe kama ataweza kushiriki michuano ya Afcon ambayo itafanyika nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 19 mwaka huu. Ghana kwasasa ipo UAE kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Misri na Tunisia kabla ya kuelekea nchini Afrika Kusini.
ULIKUWA UAMUZI RAHISI KUHAMIA CHELSEA - BA.
MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Chelsea, Demba Ba amesisitiza kuwa ulikuwa ni uamuzi rahisi kusaini mkataba na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya uhamisho wake kuthibishwa na klabu hiyo mapema leo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu akitokea klabu ya Newcastle kwa uhamisho wa paundi milioni 7.5.
Ba mwenye umri wa miaka 27 ambaye atakuwepo katika benchi la wachezaji wa akiba kwa ajili ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Southampton kesho atakuwa anavaa fulana yenye namba 29. Akihojiwa nyota huyo amesema uamuzi wa kujiunga na Chelsea ulikuwa rahisi kwake haswa ikizingatiwa kuwa timu hiyo ndio mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
AZARENKA AMKWEPA SERENA WILLIAMS.
MCHEZA tenisi nyota anayeshika namba moja katika orodha za ubora wa mchezo duniani kwa upande wa wanawake, Victoria Azarenka amejitoa katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kimataifa ya Brisbane ambapo alikuwa apambane na Serena Williams. Zikiwa zimebakia dakika 30 kabla ya mchezo wake na Williams wa Marekani kuanza, Azarenka ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano ya wazi ya Australia alitangaza kujitoa baada kuumia kidole gumba katika mkono wake wa kulia. Azarenka mwenye umri wa miaka 23 raia wa Belarus amesema amekuwa na maumivu hayo kwa kipindi cha siku kumi na yamekuwa yakiongezeka ndio maana ameamua kujitoa ili apate muda wa kujitibu kabla ya kuanza kwa michuano ya Australia. Nyota huyo amesema kulikuwa na kucha ambayo ilikuwa ikimsumbua katika kidole chake gumba lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele tatizo hilo lilizidi na kumnyima raha ya kucheza kwa kiwango chake.
Thursday, January 3, 2013
PRINCE-BOATENG AWATUMIA SALAMU ZA 2013 MASHABIKI WABAGUZI.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana na klabu ya AC Milan, Kevin-Prince Boateng jana amewaongoza wachezaji wenzake kuondoka uwanjani kwa kususia mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya daraja la nne ya Pro Patria baada ya mashabiki kuwafanyia vitendo vya kibaguzi wachezaji weusi. Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs na Portsmouth alikamata mpira na kuupiga kuelekea kwa mashabiki waliofanya vitendo hivyo katika dakika ya 26 ya mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Busto Arsizio kilometa 20 kaskazini-magharibi mwa jiji la Milan. Mchezo huo ulisitishwa baada ya wachezaji wote wa Milan kuungana na Boateng kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo huku wachezaji wa Pro Patria wakijaribu kuwabembeleza ili warejee kuendelea na mchezo huo. Wachezaji weusi waliolengwa kufanyiwa vitendo hivyo kwenye mchezo huo mbali na Boateng ni pamoja na M’Baye Niang, Urby Emanuelson na kiungo wa zamani wa Portsmouth Sulley Muntari ambapo juhudi za mshehereshaji wa mchezo huo kujaribu kuwakanya mashabiki hao zilishindikana.
MOUNTAIN BIKER STANDER KILLED IN CRASH.
MWENDESHA baiskeli za milimani raia wa Afrika Kusini, Burry Stander amefariki dunia kutokana na ajali jana huko KwaZulu-Natal na taarifa hizo kuthibitishwa na Chama cha Waendesha Baiskeli nchini humo-CSA. Kwa mujibu wa CSA Stander alikuwa akirejea kutoka mazoezini katika ufukwe wa Shelly Beach ambapo aligongwa na gari na polisi wanafanyia uchunguzi tukio hilo la kusikitisha. Stander mwenye umri wa miaka 25 alikuwa mshindi wa tano katika mashindano ya Cross Country kwenye michuano ya Olympiki iliyofanyika London mwaka jana. Mbali na kushiriki michuano hiyo ya London Stander pia alishiriki mashindano kama hayo ya Cross Country katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika Beijing, China mwaka 2008 na kufanikiwa kushika nafasi ya 15 wakati huo akiwa na miaka 20.
Subscribe to:
Posts (Atom)