Wednesday, August 5, 2015

DANI ALVES AKABIDHIWA JEZI YA XAVI.

BEKI wa mahiri wa Barcelona, Dani Alves amekabidhiwa jezi namba sita iliyokuwa ikitumiwa na Xavi kufuatia kuondoka kwa kiungo huyo mkongwe katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa akivaa jezi namba 22 kwa msimu kadhaa iliyopita kwa heshima ya mchezaji mwenzake wa zamani Eric Abidal, lakini sasa ameamua kuchukua namba ya nyota huyo wa zamani wa Hispania. Kwa upande mwingine Mbrazil mwenzake Douglas yeye amepewa jezi namba mbili kufuatia kuondoka kwa Martin Montoya kwenda Inter Milan mapema kiangazi hiki huku Munir na Sandro nao wakipewa jezi za kikosi cha kwanza ambazo ni namba 17 na 16. Golikipa Marc-Andre ter Stegan anatarajiwa kuendelea kuvaa jezi namba moja, wakati golikipa aliyekuwa chaguo la kwanza msimu uliopita yeye ataendelea na namba 13. Wachezaji wapya waliosajiliwa Arda Turan na Aleix Vidal wao hawatapewa namba kwasasa mpaka hapo watakapoanza kucheza Januari mwakani.

JUVENTUS YANASA BEKI LA ATLETICO.

KLABU ya Juventus imekubali dili la kumsajili beki Guiherme Siqueira kutoka klabu ya Atletico Madrid. Beki huyo wa kimataifa wa Brazil, bado ana mkataba wa miaka mitatu na Atletico lakini ofisa mkuu wa Juventus Giuseppe Marotta na mkurugenzi wa michezo Fabio Paratici tayari wameshafikia makubaliano na klabu hiyo. Siqueira anatarajiwa kujiunga na mabingwa hao wa Serie A kwa mkopo wa msimu mzima lakini wanaweza kumchukua moja kwa moja mwishoni mwa msimu ujao kwa kitita cha euro milioni 10. Kilichobakia sasa ni kwa Juventus kuafikiana makubaliano binsfi na mchezaji mwenyewe ambaye anadhaniwa kuwa atahitaji kulipwa kitita cha euro milioni mbili kwa mwaka.

TERRY ANATAKA KUFUATA NYAYO ZA GIGGS.

BEKI wa Chelsea, John Terry amedai kuwa amekuwa akifanya mazoezi kwa bidii kwa miaka kadhaa ili kujiweka fiti kwani anataka kucheza soka kwa kipindi kirefu kama ilivyokuwa kwa kiungo wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs. Giggs aliamua kutundika daruga akiwa na umri wa miaka 40 baada ya kuitumikia United kwa kipindi cha miaka 23 na kupewa kibarua cha kocha msaidizi wa timu hiyo akiwa chini Louis van Gaal msimu uliopita. Terry mwenye umri wa miaka 34 amekuwa sehemu muhimu katika kikosi cha Chelsea kilichotwaa taji la Ligi Kuu msimu uliopita na bado ana mipango ya kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kipindi kirefu kijacho. Akihojiwa Terry amesema katika kipindi cha miaka minne mitano iliyopita amekuwa akifanya kazi ya ziada sio katika mazoezi ya uwanjani pekee bali pia nje ya uwanja na kuhakikisha anakula chakula sahihi. Beki huyo aliendelea kudai kuwa anafanya hivyo kwakuwa anajua kuna nafasi ya kucheza kwa kipindi kirefu kama ilivyokuwa kwa Ryan Giggs.

CLARK ASAINI MIAKA MITANO VILLA.

BEKI wa Ciaran Clark amefuata nyayo za beki mwenzake Nathan Baker kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu ya Aston Villa. Baker alisaini mkataba mpya ambao utamalizika mwaka 2019 wiki iliyopita na Clark naye amekubali kusaini mkataba mwingine wa miaka mitano zaidi. Clark mwenye umri wa miaka 25 ambaye ametokana na matunda ya shule ya vijana ya Villa, amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo katika msimu ya karibuni. Nyota huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland alianza kucheza katika mechi 22 za Ligi Kuu msimu uliopita kabla ya kupata majeruhi yaliyokatisha msimu wake Aprili mwaka huu.

Tuesday, August 4, 2015

HABARI PICHA: OUT AND ABOUT, SCHWEINSTEIGER NA SCHNEIDERLIN WAKITOKA OUT NA WAPENZI WAO.


Kiungo mpya wa Manchester United Bastian Schweinsteiger akiwa na mpenzi wake ambaye ni mchezaji nyota wa tenisi Ana Ivanovic katika mtoko wao hivi karibuni.

Morgan Schneiderlin naye akiwa na mahabuba wake Camille Sold katika mtoko huo wa chakula cha usiku.

HABARI PICHA: RONALDO AJIFANYA HOMELESS NA KUTINGA MTAANI KUONYESHA UFUNDI WAKE.

Cristiano Ronaldo akitengenezwa kabla ya kuingia mtaani.



Hapa tayari akiwa mtaani akionyesha ufundi wake lakini hakuna yeyote aliyekuwa na habari naye.

Hapa sasa baada ya Ronaldo mwenye kutoa mask watu ndio wakaanza kumjalia kuomba saini yake.

INIESTA NDIO NAHODHA MPYA BARCELONA AKICHUKUA NAFASI YA XAVI.

KLABU ya Barcelona, imetangaza kuwa Andres Iniesta atachukua nafasi ya Xavi kama nahodha mpya wa timu hiyo. Mshambuliaji nyota Lionel Messi atakuwa nahodha namba mbili kwa msimu wa 2015-2016 baada ya kufunga mabao 56 katika mechi 56 msimu uliopita. Messi atafuatiwa na Sergio Busquet huku Javier Masherano akiwa nahodha namba nne. Uteuzi huo umefanyika kufuatia kura za siri zilizopigwa miongoni mwa wachezaji ambao ndio waliopendekeza Iniesta kuwaongoza msimu ujao. Gerard Pique ndiye aliyekuwa nahodha namba nne msimu uliopita lakini nafasi yake hivi sasa inachukuliwa na Muargentina Mascherano ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa manahodha kwa mara ya kwanza toka alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2010. Iniesta sasa ndio anakuwa mchezaji aliyeitumikia Barcelona kwa kipindi kirefu zaidi toka alipoibuka katika kikosi cha kwanza katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bruges, Octoba mwaka 2002.