Friday, June 29, 2012

BOLT, BLAKE NA POWELL WAKARIBIA KUFUZU OLIMPIKI.

Usain Bolt.

WANARIADHA nyota wa mbio fupi wa Jamaica Usain Bolt, Yohan Blake na Asafa Powell wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mbio za taifa za kufuzu michuano ya Olimpiki kwa mwaka huu. Bingwa mtetezi wa michuano ya olimpiki Bolt alitumia muda wa sekunde 10.06 akitanguliwa na Blake aliyetumia muda wa sekunde 10.00 wakati Powell alishika nafasi ya tatu kwakutumia muda wa sekunde 10.19. Nusu fainali na fainali ya mbio hizo inatarajiwa kufanyika baadae leo katika Uwanja wa Taifa jijini Kingston ambapo washindi watatu ndio watakaofuzu michuano ya olimpiki ambayo itafanyika jijini London. Bolt anayeshikilia rekodi ya dunia ambaye alishinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na 400katika michuano iliyofanyika Beijing mwaka 2008 ndio anayeshikilia rekodi ya mkimbiaji mwenye kasi kwa mwaka huu baada ya kutumia muda wa sekunde 9.76 katikambio zilizofanyika jijini Rome mwezi uliopita. Mkimbiaji nyota wa Uingereza Dwain Chambers alifanikiwa kufuzu michuano hiyo baada ya kutumia muda wa sekunde 10.25 wakati kwa upande wa Marekani Justin Gatlin na Tyson Gay wote walifanikiwa kufuzu wakitumia muda wa sekunde 9.80 na sekunde 9.86.

Italy Vs Germany 2-1 All Highlights And Goals 6-28-2012

Thursday, June 28, 2012

ROONEY AAMUA KUPOTEZA MAWAZO JIJINI LOS ANGELES, MAREKANI.

Ashley Cole akipita kuwasabahi kina Rooney katika hoteli hiyo.
Rooney na mkwewe wakiota jua huku wapata vinywaji katika bwawa la kuogelea.
Wayne Rooney akiwa na mkwewe Coleen katika bwawa la kuogelea katika hoteli moja iliyopo jijini Los Angeles.


BARCELONA YAPATA MBADALA WA ABIDAL.

KLABU ya Barcelona imejipanga kujizatiti kwenye safu ya ulinzi msimu ujao baada ya kufanikiwa kupata mbadala wa aliyekuwa beki wa klabu hiyo Eric Abidal ambaye ni mgonjwa kwa kumsajili beki wa klabu ya Valencia Jordi Alba kwa mkataba wa miaka mitano. Katika taarifa za klabu hiyo ambazo zimetumwa katika mtandao wa kijamii wa twitter Alba mwenye miaka 23 ambaye kabla ya kwenda Valencia alikulia katika shule ya watoto ya Barcelona amesajiliwa kwa ada ya euro milioni 14 baada ya kufaulu vipimo vya afya. Barcelona imekuwa sokoni kwa kipindi kirefu ikijaribu kutafuta beki ambaye ataziba pengo la Abidal ambaye amefanyiwa upasuaji wa kupandikiza ini mapema mwaka huu na haijulikani kama beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa atarejea tena uwanjani baada ya kupona. Alba ambaye pia yuko katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania alianza kuichezea nchi hiyo Octoba mwaka jana ambapo aliitwa kuziba pengo la Joan Capdevila katika mchezo dhidi ya Scotland na toka kipindi hicho hajaachwa kwenye kikosi hicho.

BECKHAM ATEMWA KIKOSI CHA OLIMPIKI.

KIUNGO wa kimataifa wa Uingereza ametemwa katika kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London mwaka huu. Beckham mwenye ana umri wa miaka 37 amewahi kuwa nahodha wa nchi kipindicha nyuma na alikuwa akitaka nafasi katika kikosi hicho kitakahoshiriki olimpiki kabla ya kuamua kutundika daluga. Akihojiwa mara baada ya kutangazwa kwa kikosi hicho Beckham amesema kuwa amesononeshwa na kuachwa kwake kwenye kikosi hicho lakini bado ataendelea kuwa mshabiki wa timu hiyo katika michuano hiyo na anaamini wataibuka kidedea na kunyakuwa medali ya dhahabu. Kocha wa kikosi hicho Stuart Pearce alimuingiza mchezaji huyo katika orodha ya wachezaji 35 lakini katika mchujo ili kubakia na kikosi cha mwisho cha wachezaji 18 kocha huyo alimchagua beki Micah Richards badala yake. Pearce alimpigia simu Beckham kumtaarifu hatomjuisha katika kikosi hicho kwakuwa alikuwa akihitaji kutengeneza kikosi ambacho kitakuwa cha kujihami zaidi katika michuano hiyo ndiyo maana akaamua kumchukua beki Manchester City Richards ili kusaidia kwenye suala la ulinzi.

WAARABU KUMLIPA GYAN PAUNDI 140,000 KWA WIKI.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana na klabu ya Sunderland, Asamoah Gyan anatarajiwa kusaini mkataba wa kudumu wa miaka mitano na klabu ya Al Ain ya Falme za Kiarabu-UAE ambako alikuwa akicheza kwa mkopo ambapo atakua akilipwa paundi 140,000 kwa wiki na klabu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na gazeti moja la michezo nchini Ghana klabu ya Sunderland itavuna kiasi cha paundi milioni 21 kutoka kwa Al Ain kwa kumnyakuwa mshambuliaji huyo moja kwa moja ambaye mkataba wake wa mkopo ulikuwa unamalizika msimu huu. Mkataba huo mnono utakuwa umeipa faida kubwa Sunderland ambao walinyakuwa mshambuliaji kutoka klabu ya Rennes ya Ufaransa kwa ada ya paundi milioni 13 baada ya kung’aa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ghana. Baada ya kutua Sunderland aliwashtusha wadau soka pale alipokubali klabu hiyo kumtoa kwa mkopo kwenda klabu ya Al Ain kwa ada ya paundi milioni 6 Septemba mwaka 2011 ambapo akiwa huko alifanikiwa kushinda mabao 27 katika michezo 24 liyocheza na kuiwezesha klabu hiyo kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu ya huko ambayo inafahamika kama Pro League.

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF LEO.

ILALA YAENDELEA KUGAWA POINTI COPA
Ilala imeendelea kufanya vibaya kwenye michuano ya Copa Coca-Cola baada ya leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu) kuchapwa mabao 4-0 na mabingwa watetezi Kigoma katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam. Mabao yote katika mechi hiyo ya kundi A yalifungwa kipindi cha kwanza huku Ramadhan Salum akipiga hat trick (mabao matatu). Alifunga mabao hayo dakika ya 13, 43 na 45. Bao la pili kwa washindi lilifungwa dakika ya 19 na Athuman Rashid. Wakati Kigoma imeshinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza mpaka sasa katika kundi hilo, Ilala imepoteza mechi zote tatu ilizocheza. Ilala imefungwa na Arusha, Kigoma na Lindi wakati mechi yake inayofuata itakuwa Juni 30 mwaka huu dhidi ya Kusini Pemba. Nayo Kilimanjaro imeendelea kufanya vizuri katika kundi lake la D baada ya leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu) kuitandika Shinyanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Mabao ya Kilimanjaro ambayo hadi sasa imeshinda mechi mbili na kutoka sare moja yalifungwa na Adam Soba dakika ya 11 na 46 wakati la tatu lilifungwa dakika ya 81 na James Henry. Katika mechi nyingine zilizochezwa leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu), Temeke na Mtwara zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Ali Makalani alianza kuifungia Temeke na baadaye Adam swaleh akaisawazishia Mtwara. Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani ulishuhudia Morogoro na Kaskazini Pemba zikitoka sare ya bao 1-0. Amin Kassim aliifungia Kaskazini Pemba dakika ya 51, na Morogoro wakasawazisha dakika ya 75 kupitia kwa Mutalemwa Katunzi katika mechi hiyo ya kundi B. Mechi zitakazochezwa leo jioni (Juni 28 mwaka huu) ni Lindi vs Arusha (Tanganyika Packers), Manyara vs Mjini Magharibi (Nyumbu), Kinondoni vs Mbeya (Tamco) na Kusini Unguja vs Pwani (Karume). Kesho (Juni 29 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea tena Juni 30 mwaka huu kwenye viwanja vyote vinne.


VODACOM KUKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI JUNI 30
Kampuni ya Vodacom itakabidhi zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2011/2012 katika hafla itakayofanyika Juni 30 mwaka huu kwenye hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo itakayohudhuriwa na wawakilishi wawili kutoka katika klabu ya Ligi Kuu itaanza saa 12 jioni. Katika hafla hiyo washindi mbalimbali wakiwemo bingwa, makamu bingwa na mshindi wa tatu. Wengine watakaozawadiwa ni mfungaji bora, kipa bora, timu bora yenye nidhamu, mchezaji bora wa ligi, refa bora na kocha bora.