Monday, October 31, 2011

BALE AIPAISHA TOTTENHAM.

MABAO mawili ya Gareth Bale yalihakikishia ushindi Tottenham Hotspurs wa mabao 3-1 dhidi ya Queens Park Rangers na kuifanya timu hiyo kucheza mchezo wa saba mfululizo bila kufungwa.Katika mchezo huo uliomilikiwa kwa kiasi kikubwa na Spurs, Bale aliipatia timu yake bao la kuongoza kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la hatari baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Aaron Lennon. Spurs waliendeleza mashambulizi langoni mwa wapinzani wao ambapo Rafael van der Vaart aliweza kuvunja mtego wa kuotea na kuachia mkwaju uliompita mlinda mlango wa QPR Paddy Kenny baada ya kuuwahi mpira uliokuwa umepigwa na Ledley King
QPR walichachamaa kipindi cha pili na Jay Bothroyd aliyeingia kipindi hicho aliweza kurudisha uhai kwa timu yake kwa kufunga bao la kichwa karibu kabisa na lango.Msumari wa mwisho katika jeneza la QPR ulipigiliwa na Bale katika dakika ya 72, kwa matokeo hayo Spurs wamechupa hadi nafasi ya tano mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza wakiwa wamefungana pointina Chelsea na Newcastle.

No comments:

Post a Comment