Saturday, October 8, 2011

NIGERIA YAUNGANA NA CAMEROON NA MISRI KUTOLEWA KATIKA MICHUANO YA AFCON 2012.

AFCON 2012
ANGOLA, Ghana, Guinea, Libya na Zambia zimekata tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika 2012 Jumamosi hii wakati Nigeria wakitolewa katika kinyang'anyiro hiyo baada ya kukubali bao la kusawazisha lilifungwa dakika za mwisho dhidi ya timu ya Guinea.

Mabao ya mapema yaliyofungwa na Asamoah  Gyan na John Mensah yaliisaidia Ghana kuibuka na ushindi dhidi ya Sudan na kupelekea kuongoza kundi lake kwa kuwa na pointi 16 katika michezo sita walizocheza.

Ibrahima Traore alisawazisha bao dakika ya mwisho ya mchezo na kuifanya timu yake kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi Nigeria katika mchezo uliokuwa wa kusisimua uliochezwa mjini Abuja. Guinea ndio walioanza kupata bao kupitia Ismael Bangura kabla ya Obinna Nsofor na Ikechukwu Uche kuifungia Nigeria.

Ni mara ya kwanza kwa Nigeria kutokushiriki michuano hiyo katika kipindi cha miaka 26 toka mwaka 1986.

Nigeria sasa wanaungana mabingwa wa zamani ambao nao wametolewa katika michuano hiyo ambao ni Cameroon na Misri.

Timu zilizojikatia tiketi ya kucheza michuano hiyo mpaka sasa ni Gabon, Equatorial Guinea ambao ndio waandaaji, Niger, Angola, Botswana, Côte d’Ivoire, Ghana, Guinea, Mali, Senegal, Tunisia, Zambia, Burkina Faso,  and Libya.

Michezo mingine ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika itachezwa leo ambao timu ya Taifa ya Tanzania itatupa karata yake ya mwisho itapomenyana na Morocco katika mji wa Marrakech jioni ya saa 1:30 kwa saa za kule ambapo huku itakuwa saa 4:30 usiku. Mungu Ibariki Taifa Stars Mungi Ibariki Tanzania.

No comments:

Post a Comment