RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) LEODGAR CHILA TENGA amesema wanatarajia kuwasilisha malalamiko yao katika shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA juu wa vilabu kutoka nje ya Nchi kushindwa kuwaruhusu wachezaji kuja kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars pindi wanapohitajika.
Hatua hiyo imekuja kufuatia timu ya Vancouver Whitecapes ya Canada anayoichezea Nizer Khalfan pamoja na timu ya DT LONG kutoka nchini Vietnam anayoichezea DANNY MRWANDA kushindwa kuwaruhusu wachezaji wake kuja kujiunga na Stars.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo TENGA amesema imekuwa ni kawaida kwa timu hizo kuwazuia wachezaji wao kuja kujiunga na Stars mara wanapokuwa wanahitajika hivyo wameamua kuwasilisha malalamiko yao FIFA.
Katika hatua nyingine Stars itawakosa wachezaji VICTOR COSTA pamoja na JUMA NYOSO kutokana na kukabiliwa na maumivu.
Kocha mkuu wa Stars JAN PAULSEN amesema NYOSO anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria huku COSTA akikabiliwa na maumivu ya nyonga hivyo kuwalazimu kubakiia nchini kwa matibabu zaidi.
Tayari Stars imemkosa nahodha na mlinzi namba moja wa timu hiyo SHADRACK NSAJIGWA kutokana na kuwa majeruhi.
Timu hiyo inatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea nchino Morocco kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment