Jack Warner (kushoto) akiwa na Mohamed Bin Hammam |
SAKATA la aliyekuwa mgombea wa kiti cha Urais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Mohamed Bin Hammam limechukua sura mpya baada ushahidi wa video unaomwonyesha aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Jack Warner akiwashawishi wajumbe wa Shirikisho la Soka la Caribbean (CFU) kupokea zawadi kutoka kwa mgombea huyo.
Maelezo ya Warner yaliyorekodiwa aliyokuwa akiwapa wajumbe wa CFU Mei 11 mwaka huu ndio yatakayotumika kama ushahidi katika Kamati ya Maadili ya FIFA kusikiliza mashtaka dhidi ya wajumbe hao wiki hii.
Picha ya video ambayo imechapishwa katika mtandao wa Telegraph unaonyesha Warner akiwaambia wajumbe wa CFU hawalazimishwi kumpigia kura Bin Hammam katika uchaguzi wa urais wa FIFA lakini amemwambia aje na fedha.
Bin Hammam alifungiwa maisha kujishirikisha na shughuli zozote zinahusiana na mchezo wa soka Julai mwaka huu na Kamati ya Maadili ya FIFA lakini amekata rufaa.
Hotuba hiyo ya Warner aliitoa alipokuwa Trinidad siku baada ya kukabidhiwa zawadi ya dola 40,000 kwa kila kiongozi wa CFU.
"Wakati Mohamed Bin Hammam anataka kuja huku alikuwa anataka kuleta mapambo ya fedha, vikombe vya mbao na zawadi nyinginezo na kaniambia kuleta zawadi hizo kwa watu 30 itakuwa ni mzigo mkubwa. alisikika Warner katika video iliyotolewa.
"Nikamweleza hahitaji kuleta chochote lakini kama atahitaji kuleta chochote alete kitakacholingana na zawadi alizotaka kuleta. Nikawambia kama akija na fedha sitahitaji umpe mtu yoyote lakini kama ukitoa uwape viongozi wa CFU na wao ndio watazigawa kwa wajumbe. Kwasababu sitaki ieleweke kuwa unajaribu kuwanunua wajumbe hao ili wakupigie kura na alikubaliana nami." amesema wana katika sehemu ya taarifa hiyo ya mkanda wa video.
Warner pia alisema atarudisha fedha kama viongozi hawatazichukua.
No comments:
Post a Comment