Monday, November 7, 2011
DEL BOSQUE AITA KIKOSI CHA KUIVAA UINGEREZA.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Hispania Vicente Del Bosque amemuita tena kiungo wa Sevilla Jesus Navas katika kikosi chake kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uingereza utakaochezwa Wembley Jumamosi pamoja na Costa Rica siku tatu baada ya mchezo huo. Navas mwenye umri wa miaka 25 alicheza katika fainali za Kombe la Dunia zilizopita ambapo alitoa msaada katika bao alilofunga Andres Iniesta katika mchezo wa fainali lakini Del Bosque hakumjuisha katika kikosi hicho toka alipomwita mwezi Machi mwaka huu katika mchezo wakutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya. Kikosi hicho na timu wanazotoka katika mabano kitakuwa na Makipa: Iker Casillas (Real Madrid), Victor Valdes (Barcelona), Pepe Reina (Liverpool). Mabeki: Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Raul Albiol (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Carles Puyol (Barcelona), Jordi Alba (Valencia), Ignacio Monreal (Malaga). Wakati viungo ni Xabi Alonso (Real Madrid), Cesc Fabregas (Barcelona), Sergio Busquets (Barcelona), Santi Cazorla (Malaga), Xavi (Barcelona), Javi Martinez (Athletic Bilbao), Andres Iniesta (Barcelona) na washambuliaji David Silva (Manchester City), David Villa (Barcelona), Fernando Torres (Chelsea), Fernando Llorente (Athletic Bilbao), Juan Mata (Chelsea), Jesus Navas (Sevilla)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment