Saturday, November 12, 2011

ESPERANCE WATAWADHWA MABINGWA WAPYA WA AFRIKA.

TIMU ya Esperance ya Tunisia imefanikiwa kuifunga Wydad Casablanca ya Morocco kwa bao 1-0 na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Rades jijini Tunis. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Casablanca timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana hivyo kupelekea Esperance kutawadhwa mabingwa wapya wa michuano hiyo baada ya kufanikiwa kushinda mchezo huo wa pili. Bao la Esperance liliwekwa kimiani na beki wa kimataiafa kutoka Ghana Harrison Afful dakika ya 22 na kuihakikishia timu yake ubingwa wa pili wa michuano hiyo mara ya mwisho wakiwa walichukua mwaka 1994. Mbali na kikombe Esperance wamekunja kitita cha dola milioni 1.5 na ndio wataoiwakilisha Afrika katika michuano ya Klabu bingwa ya dunia itakayofanyika Japan mwakani.

No comments:

Post a Comment