Thursday, November 10, 2011
GABON KUCHEZA NA BRAZIL KATIKA UZINDUZI WA UWANJA WAKE MPYA.
KOCHA wa timu ya Taifa ya Gabon Gernot Rohr anaamini mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Brazil utakuwa ni kipimo tosha kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuanza mapema mwakani. Gabon ndio waandaji wa michuano hiyo ya Mataifa ya Afrika wakishirikiana na Equatorial Guinea ambapo leo watazindua uwanja wao mpya uliopo Libreville kwa mchezo dhidi ya Brazil. Rohr amesema mchezo huo utaisaidia timu hiyo kuonyesha kuwa wanaweza kuzidhibiti timu kubwa ambapo katika michezo yake ya hivi karibuni timu hiyo ilitoa sare na timu za Niger na mabingwa wa zamani wa michuano hiyo Morocco na Tunisia. Kocha huyo alikuwa akilalamika kuwa timu hiyo inakosa mechi za kujipima nguvu za nyumbani na kulazimika kwenda ugenini kutokana na matengezo yaliyokuwa yakiendelea katika viwanja hivyo mbalimbali nchini humo. Hivyo kukamilika kwa uwanja huo uliopo katikati ya mji mkuu wan chi hiyo kutaipa nafasi timu hiyo kucheza mchezo wa kwanza wa kujipima nguvu na Brazil wakiwa nyumbani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment