Wednesday, November 23, 2011

TANZANIA YAZIDI KUPOROMOKA VIWANGO VYA FIFA.

TANZANIA imeendelea kuporomoka katika viwango vya ubora vinavyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kushuka nafasi tatu. Awali Tanzania iliporomoka hadi nafasi ya 131 lakini bado imeonekana kushuka zaidi katika viwango hivyo hadi nafasi ya 136 katika viwango vilivyotolewa leo. Kwa upande wan chi zingine za Afrika kuna mabadiliko katika timu zinazoshika nafasi tano za juu kwa ubora Afrika ambapo Ghana na Algeria zimepanda nafasi mbili 29 na 31 huku Misri wakiporomoka hadi nafasi ya 31. Hispania bado inaongoza katika orodha hiyo pamoja na kupoteza mchezo wao na Uingereza wakifuatiwa na Uholanzi, Ujerumani, Uruguay, Uingereza, Brazil, Ureno, Croatia, Italia na Argentina kukamilisha orodha ya timu 10 bora katika viwango hivyo.

No comments:

Post a Comment