Thursday, January 12, 2012

GHANA, IVORY COAST ZAFUKUZIA KUKATA KIU YA MUDA MREFU KUNYAKUWA TAJI LA AFCON.

Derek Asamoah
Vinara wanaoongoza soka la Afrika hivi sasa timu ya Ghana na Ivory Coast zina kiu ya muda mrefu ya kunyakuwa taji la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Ni miaka 30 imepita tangu timu ya Ghana maarufu kama Black Stars kunyakuwa taji nne la michuano hiyo huku wenzao Ivory Coast ikiwa ni miaka 20 imepita tangu wanyakue taji pekee mpaka sasa. Timu hizo zitajitupa katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 21 ambayo imeandaliwa kwa pamoja na Equatorial Guinea na Gabon ambapo timu 16 zinatarajiwa kujitupa uwanjani. Wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa utabiri wao wa nani atanyakua kombe hilo ambapo kocha wa Ghana Goran Stevanovic yeye aliipa nafasi mali wakati kiungo wa Ivory Coast anaamini kuwa Morocco na Burkina Faso zitakuwa tishio katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment