Thursday, February 2, 2012
AL AHLY KUOMBOLEZA SIKU TATU.
KLABU ya Al Ahly ya Misri imetangaza siku tatu za maombolezo kufuatia vifo vya mashabiki 70 waliokufa wakati wa mchezo baina ya timu hiyo na El Masry katika Uwanja wa Port Said jijini Cairo. Baada ya El Masry kuifunga Al Ahly ambapo ni kubwa nchini humo kwa mabao 3-1 mamia ya mashabiki wa timu iliyoshinda walivamia uwanja na kuanza kuwapiga wachezaji wa timu pinzani, mashabiki na askari waliokuwa wakilinda usalama. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imesema kuwa wameamua kusimamisha shughuli zote mpaka hapo watakapomaliza siku tatu za maombolezo. Al Ahly ambayo inajukana kwa jina la utani Klabu Nyekundu ilianzishwa mwaka 1907 na kuwa klabu yenye mafanikio zaidi katika nchi hiyo na Afrika ikiwa imeshinda Kombe la Ligi Kuu ya nchi hiyo mara 35 na Ligi ya Mabingwa Afrika mara sita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment