Wednesday, February 8, 2012

AL AHLY KUTENGEZA JEZI NYEUSI.

TIMU ya Al Ahly imeagiza kampuni ya Adidas ya Ujerumani kuwatengenezea jezi za rangi nyeusi ambazo watazitumia kumalizia msimu wa Ligi Kuu nchini Misri. Chanzo kimoja cha habari kilisema pia timu hiyo itaagiza fulana maalumu zenye rangi nyeusi kwa ajili mashabiki wa timu hiyo lakini tarehe kamili ya kuwasili kwa vifaa hivyo haikuwekwa wazi. 
Fahim Omar
Kwasasa mwamuzi aliyechezesha mchezo baina ya Al Masry na Al Ahly Fahim Omar ameeleza kuwa bado anaendelea kupokea vitisho vya kuuwawa kutoka kwa watu mbalimbali baada ya mchezo huo. Omar alikiri kuwa wachezaji wa Al Ahly Mohamed Barakat na Hossam Ghaly walimuomba mwamuzi asimamishe mchezo huo baada ya mashabiki kuanza kurusha mafataki lakini hakufanya hivyo akijua hali hiyo ingetulia.

No comments:

Post a Comment