Sunday, February 5, 2012

BOATENG AWAONYA WENZIE KUHUSU MATUTA.

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya Ghana anayecheza soka la kulipwa nchini Ukraine katika klabu ya FC Dnipro Derek Boateng amewaonya wachezaji wenzake katika timu hiyo kuepuka kufikia hatua ya changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika utakaochezwa leo. Boateng aliwataka wachezaji wenzake kumaliza kazi mapema katika dakika 90 za muda wa kawaida au katika dakika 30 za nyongeza ambapo kama wakienda sare dakika zote hizo 120 basi changamoto ya mikwaju ya penati ndio itakayoamua mshindi. Ghana ambao wanajulikana kwa jina la utani la Black Stars au Nyota Weusi walishindwa kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutoka bara ya Afrika kuingia hatua ya nusu fainali katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 baada ya kupoteza kwa Uruguay. Kumbukumbu hizo zikiwa bado hazijafutika kichwani Boateng ametaka wachezaji wenzake kutumia nafasi zitakazotengeza vyema ili kupata mabao katika mchezo wao wa dhidi ya Tunisia.

No comments:

Post a Comment