Sunday, February 5, 2012
HALI MBAYA YA HEWA ULAYA YASABABISHA SERIE A KUSIMAMA.
LIGI Kuu nchini Italia-Serie A imesimamishwa tena kutoka hali mbaya ya hewa iliyozikumba nchi nyingi za Ulaya ambapo kumekuwa na barafu nyingi sana ikidondoka. Mchezo kati ya Inter Milan na Roma ambao ulikuwa uchezwe Jumamosi umesogezwa mbele mpaka Jumapili kutokana na barafu nyingi ambayo ilikuwa ikidondoka katika mji mkuu wan chi hiyo Rome. Barafu ilianza kudondoka kwa kasi Ijumaa mchana katika jiji hilo na katika kipindi kifupi mabonge makubwa ya barafu yalikuwa yamefunika sehemu kubwa ya mitaa ya jiji hilo hivyo kuwafanya polisi kusogeza mbele mchezo huo mpaka Jumapili mchana ambapo hali itakuwa imetengemaa kidogo. Mchezo mwingine uliokuwa uchezwe Jumamosi kati ya Cesena na Catania nao umesogezwa mbele baada ya barafu kudondoka kwa wingi katika Uwanja wa Dino Manuzzi na kufikia futi mbili na hakuna tarehe yoyote iliyotajwa kwa ajili ya mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment