Tuesday, March 6, 2012

FIFA KUSOGEZA MBELE MECHI ZA KIRAFIKI ZA KIMATAIFA.

SHIRIKISHO la Soka duniani-FIFA linataka kuondoa michezo ya kimataifa ya kirafiki ambayo huchezwa Februari na Agosti kitendo ambacho kinaonekana ni kama kuziridhisha klabu za Ulaya. FIFA tayari imeshatangaza mapendekezo ya kalenda hiyo kwa mwaka 2015-2018 ingawa mpaka sasa hakuna tarehe maalumu iliyotajwa kwa ajili ya michezo hiyo. Kalenda iliyopendekezwa itazihitaji timu za taifa kucheza michezo miwili kila moja mwezi Machi, Septemba, Octoba na Novemba ukiongeza na June katika miaka ambayo haigawanyiki. Kama kalenda hiyo ikipitishwa bara la Amerika Kaskazini, Kati pamoja na nchi za Caribbean zinaweza kulazimika kufanya mabadiliko ya michezo yao ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018.

No comments:

Post a Comment